Maendeleo juu ya kinga/chanjo dhidi ya virusi vya Ukimwi (HIV/AIDs), ukilinganisha na Covid-19.

Written by: Dr. Amani Albert

Posted at: 2021-03-02 12:57:08


Wakati dunia ikielekeza nguvu na rasilimali nyingi katika kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid-19) maendeleo dhidi ya kutafuta chanjo/kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi (HIV/AIDs) yamedorora. Wakati ukweli wa kwamba mafanikio katika kutengeneza chanjo ya kudhibiti virusi vya Corona (Covid-19) yametokana sana na miaka 20 ya utafiti na maendeleo katika kutafuta chanjo dhidi ya virusi vya Ukimwi (HIV/AIDs), dunia imeonekana kuelekeza nguvu nyingi katika kupambana na Corona kuliko Ukimwi. (Ugonjwa ambao umesumbua dunia kwa zaidi ya miaka 40) Ukulinganisha magonjwa haya mawili; 1. Ugonjwa wa Ukimwi (HIV/AIDs) umeonekana kuadhiri Waafrika zaidi kuliko watu wengine wote duniani. Katika jumla ya idadi ya vifo milioni 32 vilivyo sababishwa na Ukimwi duniani asilimia zaidi ya 75% ya vifo vimetokea Afrika peke yake, ya watu zaidi ya milioni 24. Wakati vifo vilivyo sababishwa na ugonjwa wa Corona Afrika ni chini ya asilimia 5% dunia nzima. 2. Asilimia 69% ya watu wanaishi na virusi vya Ukimwi wanatokea Africa. 3. Asilimia 91% ya watoto wanaoishi na Ukimwi duniani wanatokea Afrika peke yake. 4. Mwaka 2019 watu 700,000 wamefariki kutokana na virusi vya Ukimwi, watu 470,000 wakitokea Afrika (zaidi ya asilimia 67%). 5. Ugonjwa wa Corona (Covid-19) umepokea mara ×8 zaidi ya fedha (funding) kuliko ugonjwa wa Ukimwi katika kupambana nao. Fedha zikienda katika kufadhili chunguzi mbali mbali, tiba na chanjo. 6. Kinga/Chanjo dhidi ya Corona imepatikana ndani ya mwaka mmoja katika kutengeneza, majaribio mpaka kupewa leseni, wakati utafiti dhidi ya virusi vya Ukimwi ukichukua zaidi ya miaka 20. Katika magonjwa yote haya mawili, yote ni hatari na hakuna wenye afadhali. Pamoja ya kwamba chunguzi dhidi ya kinga/chanjo ya Ukimwi umepiga hatua sana, lakini Je ni kwasababu Ugonjwa wa Ukimwi hau adhiri zaidi mataifa yalio endelea ukilinganisha na Afrika ndio maana nguvu nyingi haiwekezwi huko ???



Read more and consult the doctor on LyfPlus Mobile App.